Fid Q
Farid Kubanda (amezaliwa tar. 13 Agosti 1982, katika
hospitali ya Bugando iliyopo jijini Mwanza) ni msanii wa hip hop na Bongo Flava
kutoka nchini Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Fid Q.
Historia
Shughuli za awali (kwa ufupi)
Fid Q alianza
shughuli za muziki mnamo miaka ya 1990. Fid Q alitoa kibao chake cha kwanza
mwaka 2000 kiitwacho 'Huyu na Yule' ambacho hicho aliimba na msanii Mr Paul.
Kibao hiki kilimpa heshima kubwa, kibao hicho kilirekodiwa katika studio za MJ
records chini ya usimamizi wake Master Jay mwenyewe.
Kibao chake cha pili
kutoka kiliitwa 'Binti Malkia' ambacho alimshirikisha Noorelly. Ilivyofika
mnamo mwaka wa 2004 Fid Q alivunja ukimya wake kwa kibao chake mahili
kilichokwenda kwa jina la "Fid Q.com", na kibao hicho alikifanya
katika studi ya Baucha Records baada ya kuhama kwa MJ.
Kibao
hicho kiliirudisha ile hiphop ya Tanzania katika ramani yake halisi na
inasemekana hivyo kwasababu kipindi hicho ni kile ambacho wasaanii wengi wa
muziki wa kufokafoka walikuwa wamejiingiza katika masuala ya uimbaji kwasababu
kulikuwa na uvumi wa kwamba hip hop haikubaliki kwa watu wa Tanzania. .Fid
anatajwa kuwa Ni miongoni mwa wasanii walioleta heshima ya hip hop Tanzania na
Afrika mashariki na kibao chake kinachojulikana kama Mwanzamwanza kilifanya
vizuri ambapo ndani yake kuna uandishi wa kipekee ambao umeenda tofaut na ule
uliokuwa umezoeleka(masimulizi/mipasho).
Ilipofika
mwezi wa Januri ya 26 katika mwaka wa 2008, Fid Q alipakua kibao kiitwacho
"Ni Hayo Tu" alichomshirikisha Prof. J na Langa. Kibao hicho
kilibahatika kujinyakulia Tuzo ya Kili kikiwa kama kibao bora cha muziki wa hip
hop kwa mwaka wa 2007-2008.
Fid Q ana albamu
mbili kwenye soko la muziki. Albamu ya kwanza inaitwa inayoitwa "Vina
Mwanzo Kati na Mwisho". Mwishoni mwa mwaka 2009 alitoa albamu ya pili
"PROPAGANDA", ambayo imepokelewa vizuri sana Tanzania na nchi
nyingine za Afrika Mashariki. Mashabiki wa Hip Hop wanaichukulia PROPAGANDA
kama ni albamu bora kabisa, yaani 'classic'. Hivi karibuni anategemea kutoa
albamu yake ya tatu itakayokwenda kwa jina la "KitaaOLOJIA".
Marejeo:
https://sw.wikipedia.org/wiki/Fid_Q
cheusidawa.blogspot.com/p/fid-q-biography.htm
https://softkenya.com/africa/fid-q/
https://www.last.fm/music/Fid+Q/+wiki
youzeek.com/?Artist=Fid+Q&page=Biography
www.musicians4africa.com/artists/fid-q/
tiavaKin_ru German Cirulis https://wakelet.com/wake/XymSXI85xrFS0zXCoyCsN
ReplyDeletenabseiteti
Uenblanpulch_yu_Omaha Kathy Smith download
ReplyDeletelink
download
link
midpugesttur